26 Agosti 2025 - 11:18
JMAT Yatangaza Mafunzo ya Msingi ya Itifaki na Ustaarabu (J-PEC) Jijini Dar es Salaam

Taarifa zinaeleza kuwa, mafunzo hayo yatafanyika kuanzia tarehe 16 – 18 Septemba 2025, katika Ukumbi wa Nefaland Hotel Hall, Manzese – Argentina, Dar es Salaam, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kila siku.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Dar es Salaam - Tanzania, Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imetangaza kuandaa "Mafunzo ya Msingi ya Itifaki na Ustaarabu" yajulikanayo kama JMAT Protocol and Etiquette Course (J-PEC). Mafunzo hayo yamekusudiwa kutoa ujuzi muhimu kwa Taasisi za Serikali, binafsi, pamoja na wanajumuiya wa JMAT.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya JMAT, mada kuu zitakazojadiliwa katika mafunzo hayo ni pamoja na:

  1. Dhana, Malengo, Historia, Dhamira na Hadhi ya JMAT.
  2. Misingi ya Itifaki ya Uongozi na Matukio.
  3. Misingi ya Ulinzi na Usalama wa Taasisi.
  4. Dhana, Misingi, Umuhimu na Nguzo za Uzalendo.

Mafunzo hayo yatatolewa na wakufunzi waliobobea kutoka taasisi zinazoheshimika na kuaminika kitaifa.

Taarifa zinaeleza kuwa, mafunzo hayo yatafanyika kuanzia tarehe 16 – 18 Septemba 2025, katika Ukumbi wa Nefaland Hotel Hall, Manzese – Argentina, Dar es Salaam, kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kila siku.

Ada ya ushiriki kwa mafunzo haya ni Tsh. 150,000/= ambapo washiriki wote watapewa Cheti Maalum cha Mafunzo, pamoja na huduma za chakula, vinywaji na nyenzo za kielimu wakati wote wa mafunzo.

Kwa mawasiliano na usajili, waombaji wanaombwa kuwasiliana na:

📞 Mkurugenzi Mkuu: 0764 597 339 | 0744 490 340

JMAT Yatangaza Mafunzo ya Msingi ya Itifaki na Ustaarabu (J-PEC) Jijini Dar es Salaam

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha